Kutumia hukmu ya Qur'aan na Sunnah katika kila jambo la maisha yetu ya kila siku.
Kila jambo la itiqadi , ibadaah ama manhaj (mfumo wa dini) ambalo halina hoja katika Qur'aan na Sunnah , na ambalo maswahaba (radhiyaAllahu anhu) hawakukubalina wala hawakulitaja , basi jambo hilo ni upotofu na bid’a (uzushi) . Tunalikataa na kujiweka mbali nalo.
Tunamuabudu Allah kwa kukamilisha Tawheed . Hatuombi yeyote ispokuwa Allah na hatujilindi na yeyote isopokuwa Allah .Na Katika mambo ya ibada hii ni : kuwachukuia washirikina.
Kuwa tahadharisha na kuwaonya waislaamu kutokana na madhara na ubaya wa shirk na mifumo yake mengi. Pamoja Na kuwaita kuregea katika Tawheed . Yeyote anayeshikilia katika ushirkina baada ya hapo , basi tunaji tenga naye na tunamchukia kwa sababu ya Allah.
Tuna amini kuwa Hukmu na sharia ya Allah imekuja kwa mifumo miwili : Qur’aan na Sunnah . Hukumu hii imekamilika . Hakuna kitu kipasacho kuongezwa juu yake , wala hukmu yeyote kupunguzwa. Yeyote anayefanya hivyo , basi amekufuru.
Tuna itaqidi mfumo (manhaj) wa kufahamu na kuzitekeleza Hukmu na Sheria za Allah , ni kupitia mfumo na mfano wa Mtume sallallaahu ‘alayhi wasallam , Maswahaba (radhiyaAllahu anhum) , na wale waliokuja baada yao ambao walifwata mwenendo huo.
Yeyote anayetaka kupata radhi na rehema ya Allah , kupitia mfumo usiokuwa wa Mtume sallallaahu ‘alayhi wasallam na Maswahaba (radhiyaAllahu anhum) basi amepotoka na ameshika njia isiyokuwa ya haki. Ame hasirika dunia hii na hio ijayo.
Kuwaonya ndugu waislaamu kutokana na : mambo ya uzushi (bid’a) , hadeeth dhaif na hadeeth mau’dhu (zilizo tungwa). Haya ndiyo katika mambo ambayo yametia ubovu katika dini safi na nzuri, pamoja na kuleta madhara katika kuendeleza ummah wa kiislaamu.
Hivyo tuna wahimiza ndugu wa islaamu waishike na wafuwate sunnah kupitia mfumo wa ahlul hadeeth (wana chuoni wa hadeeth) , hivyo tunafwata hadeeth zilizo saheeh na kujitenga na zilizo dhaif na za uzushi.
Tuna amini na kukubali Asmaa ul husna (Majina Mazuri) na Sifaat za Allah ; zote zilizo thibitishwa katika Qura’n na katika hadeeth saheeh. Tuna amini majina hayo na sifa hizo bila ya:
Usawa na haki ni kuamini na kufahamu majina na sifa za Allah kama alivyozifahamu na kuzieleza Mtume sallallaahu ‘alayhi wasallam na Maswahaba (radhiyaAllahu anhum) ; pasi na kuingia katika fikra za kuuliza vipi , na kutaka kujuwa namna ya sifa za Allah , kwani hakuna binaadamu awezaye kujuwa.
Hatushindani wala kujadiliana katika mambo ya aqeedah (‘itiqadi), wala hatutumii ufahamu wetu (usipotakikana). Tuna amini na kufwata kama vile alivyo amini Mtume sallallaahu ‘alayhi wasallam na Maswahaba (radhiyaAllahu ‘anhum) na as-salafu saalih (watu wema waliyowafwata).
Hatushindani wala kujadiliana na ahlul bid’a wal hawaa (watu wa uzushi na wenye kufuata matamanio ya nafsi zao) , hatukai nao katika vikao vyao , wala hatuwasikizi upotofu wao.
Ni lazima kwa kila mmoja wetu : kuwahishimu ma ulamaa na mashaykh wa sunnah , kuwa kirimu , na kuchukuwa ilimu kutoka kwao . Pamoja na kujilinda na kuwa shutumu na kuwasema vibaya kama wanvyofanya wapotofu.
Tuna amini kuwa haifai, kuwaendea kinyume , kuwatukana na kuwapiga vita viongozi wa kiislaamu , maadam wana simamisha swala na wanajitahidi kusimamisha sharia.
Ibada ya kumuabudu Allah ni kupitia sunnah , na kufuata haki kwa kujisalimisha kabisa. Bila ya kuchaguwa mtu mmoja ama kundi la watu ya kuwa hawa ndio wakufwata bila ya pingamizi katika kila jambo.
Mtu anayefwata bila ya pingamizi ni mmoja : Muhammad sallallaahu ‘alayhi wasallam.
Tunampenda kila muislaamu kadri ya uchaji Mungu wake na kadri ya anavyofwata Sunnah, na tunamchukia kwa kadri ya upotofu wake na kwa kadri ya upinzani wake wa Sunnah.
Tuna wapenda wanao fanya juhudi ya kusaidia Sunnah na watu wake : na tuna wachukuia wapinzani wa Sunnah na watu wa bid’a.
Tuna mahaba na tunawapenda kila mmoja katika Maswahaba wa Mtume (sallallaahu ‘alayhi wasallam). Tuna wachukia wale wano wataja kwa vibaya maswahaba. Na anaye wataja vibaya maswahaba , jihadhari naye! Huyo ni mpotofu , zindeeq.
Katika ‘Itiqadi yetu : tuna amini Qu’ran ni maneno (kalima) ya Allah . Haikuumbwa wala kutengenezwa.
Hatumtowi mtu yeyote katika watu wa qiblah(muislaamu) kutoka katika uislaamu ; kwa sababu ya dhambi zake anazozifanya . Maadam haja amini kuwa dhambi hizo ni halal.
Tunakataa kila aina ya hizbiyyah ( kujigawanya vikundi mbali na sunnah) , na tuna amini ni lazima kuwa bainisha na kujitahadhirisha na kila mpinzani wa sunnah ; bila ya kujali mfumo wake , cheo chake ama kadri ya upinzani wake wa sunnah. Tunafanya hivyo kupitia manhaj iliyowekwa katika dini. Hivyo tuna ilinda dini hii , iliyotakasika na kuuweka uzuri wake daima , inshaAllah.
Tunasema ukweli katika kila hali na kila wakati . Hatu ogopi ugomvi na shere za wapotofu. Hivyo tunafwata Sunnah na tunashikamana nayo kwa meno yetu , katika hali nzuri na hali mbaya – mpaka itakopifika amri ya Allah (siku ya kiama).