Na ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye (viumbe) kwa Mwenyezi Mungu na (mwenyewe) akatenda mema. Na akasema: “Hakika mimi ni katika Waislamu?&rduo;
[Fussilat, 41:33]
Jukumu Letu ni chama cha ufadhili, kilofunguliwa hususan kuwasaidia vijana mayatima wa kiislaamu walioko Mombasa, ambao ni:
Katika kuifahamu hali ya Mombasa, baadhi ya ndugu zetu waligutushwa kwa idadi ya vijana wanaoacha kusoma. Wengi wao wakiwa ni mayatima, wasiokuwa na uwezo wa kifedha , na wasiokuwa na usaidizi wa kihisia kuwahudumisha katika masomo yao na maisha yao. Idadi kubwa ya vijana hawa, huwa ni waislamu waliobarakiwa na ufahamu mzuri na pia mara nyingi ni : waerevu kimasomo, wenye bidii , na wana juhudi(inshaAllah) itakayo wawezesha wa faulu katika maisha yao , na kuwawezesha wapate miradi ya hali ya juu, lakini inasikitisha kuona uwezo wakufuata miradi hayo na kufikia malengo yao : hawana!
Kama kutapatikana watu wachache , wajitolee kwa sababu ya Allah ; kuchanga $10 (~£5) kwa mwezi : yatima mmoja katika Jiji la Mombasa anaweza kupata usaidizi wa ilimu, ambao unaewza kuwa sababu ya kuja akawa mtu muadilifu na muaminifu katika Ummah wetu . Mchango huu ambao unaonekana kwa wengi wetu kuwa ni kidogo, ni mkubwa sana mjini Mombasa. Na InshaAllah huenda , ukafika mbali kwa wakati na kuleta athari njema.
Kurahisisha njia za kuwaelimisha vijana wa kiislamu. Kuungana pamoja kufundishana na kusambaza mafundisho matakatifu ya kiisalamu kulingana na:
Kujitenga na kujiweka Mbali na Uhizbiyyah (kutengeneza vipote kando,visivyofuata mfumo wa maswahaba) , ghuluww (ulokole), bid’ah na ufuasi wa upotofu.